Dunga Mawe

Dunga Mawe

Kontawa

Альбом: Dunga Mawe
Длительность: 3:30
Год: 2023
Скачать MP3

Текст песни

DUNGA MAWE
Jam on the beat

Anaitwa dunga mawe
Mwanangu wa utoto
Katika kitu nakumbuka
Alipitia changamoto
Mwanangu dunga mawe
Alikuwaga kibokoo
Na sura yake ilitumika
Kutishia watoto
Eeee
Oya huyo mwanangu alikuwa msela
ALishawahi kufungwa akatoroka jela
Maisha yake visanga yani mpelampela
Asa ngoja niwape movie hilo lilikuwa twela
Eeee
Kuna kipindi dunga mawe si alipata mwali
Tukaenda hadi ukweni si kutoa mahali
Baada ya vitu kukamilika tulivyopewa mwali
Akamvizia baba mkwe akamwibia mahali

Alianza kuvata bangi na miaka saba
Ulivyofika wa nane akaanza kukaba
Sababu ya hali ngumu kakosa msaada
Eee
Hakuwahi kuwa na mama wala huyo babaa
Ndugu wa karibu hawakumpa faraja
Mali alizoachiwa na wazazi waakee kadhurumiwaa

Aaaah aah
Anaitwa dunga mawe
Aaah aaah
Mwanangu dunga mawe
Aaah aah
Anaitwa dunga maawe
Aaah aaah
Mwanangu dunga mawe

Ukimletea unyonge lazima aruke nawe
Bora ukabwe na tonge ila sio dunga mawe
Utafanya kitu gani hili umfanye apagawe
Kashaoga matusi mpaka akaamua anawe
Ile siku dunga mawe akiamka vizuri
Tena ukamkuta kwenye mood
Anaweza agiza bia mbili
Afu akakupa mia mbili
Kisha akasema kwamba chenji inarudii
Demu wake dunga mawe alikuwa na mimba
Yapata kama miez tisa
Kwa kuwa pesa ya uzazi ilimshinda
Ikabidi awe anapiganisha
Akamwambia kwamba mpenzi wake kuwa amepata safari
Anaenda kupambana hili mambo yawe shwari
Na atakaporudi watakwenda hospitali
Aaaahh
Eeee
Kumbe alipanga kwenda kuiba huko sehemu za mbali
Ndipo akakamatwa na watu wenye asira kali
Wakamshushia kipigo
Kipigo juu ya kipigo
Namwisho wakamchoma na mipira ya magari

Aaaaa aaaah
Anaitwa dunga mawe
Aaaaa aaaah
Mwanangu dunga mawe
Aaaa aaaah
Anaitwa dunga maawe
Aaaa aaah
Mwanangu dunga mawe

Alianza kuvata bangi na miaka saba
Ulivyofika wa nane akaanza kukaba
Sababu ya hali ngumu kakosa msaada
Eeeee
Hakuwahi kuwa na mama wala huyo babaa
Ndugu wa karibu hawakumpa faraja
Mali alizoachiwa na wazazi waakee kadhurumiwaa

Aaaaa aaaah
Anaitwa dunga mawe
Aaaaa aaaah
Mwanangu dunga mawe
Aaaa aaaah
Anaitwa dunga maawe
Aaaa aaah
Mwanangu dunga mawe