Nilijua Utatenda
The Christ Highlanders Chorale
4:21*NENO LA MWISHO* STANZA 1 Moyo wa mtu huifikiri njia yake lakini Bwana huongoza hatua zake Njia zote za mtu ni safi machoni pakee Lakini Bwana huzipima huzipima roho za watu Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu lakini jibu la ulimi hutoka kwa Bwana Bwana amefanya kila kitu kwa kusudi lake Japo tunayo mipango mapenzi yake yatimia Mwenye neno la mwisho ndiye akisema amesema Mwenye neno la mwisho ndiye akiamua nani apinge eh CHORUS Mkabidhi Bwana njia zako na mawazo yako yatathibitika Hakuna gumu kwa Bwana anaweza aah Japo mambo hayaendi jinsi sisi tulivyotarajia Yu mwaminifu kutimiza kazi njema aliyoanza kwetu STANZA 2 Laana walonitamkia adui siyo mwisho wangu Mashimo walonichimbia nianguke siyo mwisho wangu Na yale mabaaya waloninenea siyo mwisho wangu Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi siyo mawazo mabaya bali ya kuwapa amani na tumaini Mwenye neno la mwisho sema sema semaa juu ya kazi zetu weeeh Sema sema semaa juu ya afya zetu Bwanaa ah Sema sema semaa juu ya huduma zetu eeeh Sema sema semaaa ukiamua nani apinge eeeh CHORUS Mkabidhi Bwana njia zako na mawazo yako yatathibitika Hakuna gumu kwa Bwana anaweza aah Japo mambo hayaendi jinsi sisi tulivyotarajia Yu mwaminifu kutimiza kazi njema aliyoanza kwetu